Wafanyakazi IAA Washiriki Maadhimisho Mei Mosi Kimkoa

Watumishi wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) wameshiriki katika Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambayo kimkoa yamefanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Shekh Amri Abeid Karume, Kaloleni Jijini Arusha.

Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela, huku kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka huu ikiwa ni “Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi, Wakati ni Sasa”.